Matatizo ya meno ni matatizo au magonjwa yanayohusiana na meno, karibia matatizo yote ya meno husababisha na bakteria au wadudu wengine kuwepo mdomoni, hii hufanya mtu kuwa na maumivu makali kwenye meno na kupelekea kutoa damu au harufu mbaya na kuathiri meno.
Matatizo mengi ya meno yanazuilika na kutibika. watu wengi wana tatizo la meno ila wanatofautiana Kwa ukubwa wa tatizo. watu wanashauriwa wawe na tabia ya kuchunguza meno yao ili kujilinda na matatizo ya meno, tibu tatizo mapema ili kuepuka kuharibika na kung’oka kwa Meno.
AINA ZA MAGONJWA YA MENO
Mdomo una magonjwa mengi ila meno ndio tatizo kubwa sana na ndio linaweza kuleta na matatizo mengine, aina za magonjwa ni kama;
- Meno kutoboka
Hili ni tatizo linalotokea kwenye meno kwa kuwepo kwa bakteria kwenye meno na kuharibu meno, bakteria hao wanaweza kutokana na kuwepo kwa mabaki ya vyakula hasa vyenye sukari nyingi. Mabaki yasipoondolewa bakteria huzalisha acidi ambayo ndio huharibu meno na kutengeneza vijitobo.
- Meno kuvunjika.
Hili ni tatizo ambalo huwatokea watu wakionekana meno yao kuna baadhi na vipande kutoonekana, jino laweza kuwa nusu au robo tatu, mara nyingi hili sio tatizo hatari halina madhara makubwa kwakuwa haliathiri fizi ila linaweza kumnyima mtu uhuru wa kucheka na pia ulimi ukigusa Jono unahisi kama ni kitu chenye ncha.
- Meno kusagika au kupungua kimo
Hili tatizo hutokea ukiwa umelala, hata mchana ukiwa na mawazo, hasira au hisia ambapo meno hugusana na kusagana. Meno huweza kupungua kimo na kuisha hii hutokea kwa muda mrefu kidogo, meno yakisagika na kupunguwa kimo husababisha maumivu ya meno na kubadilika rangi.
- Tatizo la fizi
Hili ni tatizo katika fizi kuna kuwa na maumivu, kama vidonda au kutokwa damu, kuwa na usaa au uchafu. Mara nyingi hutokana na bakteria wanaokuwa kwenye mabaki ya chakula usipoyaondoa bakteria wanaanza kuvamia fisi na kuziharibu. Mtu mwenye hili tatizo hutoa harufu mbaya.
- Meno kuharibika, fizi kuachia na kulegea.
Hili tatizo ni pale meno yanapoonekana sio ya kawaida; yaani yanakuwa yamebadilika rangi, fizi kuharibika, fizi kupungua, fizi kutoka damu na meno kulegea. Hili ni tatizo ambalo laweza kuwa kubwa na kutotibika
- Meno kufa ganzi na kushindwa kuhisi
Hili ni tatizo huwakuta wengi katika mazingira ya baridi sana au joto sana, pia wakila baadhi ya vyakula vyenye uchachu, vyenye sukari na vingine. Tatizo hili ni dalili za kuharibika kwa jino ndani au nje
- Harufu mbaya na kupumua vibaya
Hili tatizo hutokea kwa mtu kutoa harufu mbaya mdomoni ambayo huwakera watu wengi, hii hutokea pale anavyokuwa na mabaki ya vyakula kwenye mdomo, kutofanyia usafi meno na mdomo pia, kuwa na tatizo la meno au mdomo.
- Meno kuoza au Utando mdomoni
Hili ni tatizo ambalo mdomoni huwa na weupeweupe usioeleweka kama ute, mara nyingi huwatokea watu wasio na kinga imara hasa wenye matatizo ya kiafya kama kisukari, UKIMWI, Kansa (Saratani), Asthma. Hii hali huondolewa na matumizi ya dawa.
- Meno kuwa na rangi ya njano, kaki au kahawia
Hili tatizo limeonekana kuchukua baadhi ya maeneo na watu wengi, ambapo idadi kubwa ya watu wameonekana wakiwa na meno yenye rangi inayoendana. Hii ni kwasababu ya vyakula na maji ya kunywa yanayopatikana maeneo hayo kuwa na uwingi wa aina flani ya madini hasa madini ya fluoride.
CHANZO CHA MAGONJWA YA MENO
Chanzo cha magonjwa ya meno kwa asilimia kubwa ni mitindo ya maisha tukimaanisha usafi, ulaji, mazingira na tabia mbalimbali, mambo yanayoweza kukusababishia kupata matatizo ya meno ni kama;
- Kutokusafisha mdomo pamoja na meno
- Ulaji holela wa vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
- Kutokupata tiba ya kisukari na ugonjwa wa moyo
- Kuvuta sigara
- Kuwa na magonjwa yanayopunguza kinga ikiwemo na UKIMWI
- Kubadilika kwa baadhi ya homoni
- Umri
- Utumiaji wa madawa yenye kemikali nyingi huharibu mfumo wa vimiminika vinavyofanya mmeng’enyo
- Historia ya magonjwa yanayoambatana na meno katika familia
- Mazingira
DALILI ZA MTU MWENYE TATIZO LA MENO
Mara nyingi dalili hujionesha wazi wengi hujijua kuwa tayari wana tatizo na mara nyingi huwa si lazima vipimo, zaidi huhitajika uchunguzi kujua chanzo. Dalili zake ni kama
- Meno kuuma wakati wa kula au mda wa baridi au joto
- Kutokwa na damu kwenye fizi
- Meno kuanza kulegea na kuachana na fizi
- Kutoa harufu mbaya mdomoni, hii huonesha kuna tatizo
- Meno kubadilika rangi mfano nyeusi, njano, kahawia na rangi zingine zisizo za kawaida
- Fizi huwa nyekundu kama damu ikiwezekana kuna na vidonda
- Mdomo kuwa mkavu
- Meno kufa ganzi
- Meno kuchomoka au kutikisika
JINSI YA KUEPUKA MAGONJWA YA MENO
- Ondoa mabaki ya chakula kwa kusukutua mdomoni na maji baada ya kutoka kula pia Kunywa maji mengi dakika 30 baada ya kupata chakula.
- Safisha meno yako hata mara mbili kwa siku
- Usivute sigara
- Punguza au acha kunywa pombe
- Kula vizuri vyakula bora hasa asilia na sio vyakula vyenye kemikali, vyakula vyenye mafuta mengi na sukari nyingi
Leave a Reply