UN waonya kuhusu kulegeza juhudi za kulinda mazingira

UN waonya kuhusu kulegeza juhudi za kulinda mazingira

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imebainisha kuwa miaka minane iliyopita inaelezea kuwa ya joto zaidi kuwahi kurekodiwa, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akionya kuwa sayari inatuma ujumbe wa kuomba msaada.

Shirika la hali ya hewa na tabianchi la Umoja wa Mataifa, jana limetoa ripoti yake ya kila mwaka kuhusu hali ya tabianchi ya dunia, ikionya kwamba shabaha ya kuweka ukomo wa ongezeko la joto la dunia kwa nyuzi 1.5 za celsius ilikuwa mbali na kufikiwa.

Wawakilishi kutoka mataifa karibu 200 wamekusanyika nchini Misri kujadili namna ya kubakisha ongezeko la joto kwa kiwango hicho, kama ilivyopendekezwa na kamati ya kiserikali kuhusu mabadiliko ya tabianchi, IPCC, lengo ambalo baadhi ya wanasayansi wanasema hivi sasa halifikiki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags