Ummy Mwalimu awatembelea majeruhi ajali ya basi la Arusha Express

Ummy Mwalimu awatembelea majeruhi ajali ya basi la Arusha Express

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amewatembelea majeruhi wa ajali ya basi la Arusha Express lililogongana na lori, katika eneo la Mzakwe, Dodoma. Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na wanaendelea vyema na matibabu.

Aidha, amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi 21 ambapo hadi kufikia leo majeruhi mmoja ambaye alipatwa na majeraha makubwa amefariki na kufanya idadi ya waliofariki kufikia watu 7, watu 9 wameruhusiwa kuondoka na 11 wanaendelea vyema na matibabu.

Hata hivyo Mhe.Ummy amewashukuru watumishi wa hospitali hiyo kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa huduma za matibabu kwa wagonjwa na majeruhi wa ajali hiyo iliyotokea.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags