Ukraine na Urusi kubadilishana wafungwa

Ukraine na Urusi kubadilishana wafungwa

Rais kutoka nchini Ukraine, Volodymyr Zelensky amethibitisha kuachiliwa kwa wafungwa wa kivita kama sehemu ya makubaliano kati ya Ukraine na Urusi.

Makubaliano hayo yamefanikisha wanajeshi 200 waliokuwa wakishikiliwa katika pande zote za mzozo kurejeshwa kwenye mataifa yao.

Zelensky amesema mpango huo umefanikisha wanaume 80 na wanawake 20 kurejea Ukraine na miongoni mwao ni pamoja na waliopambania Jiji la Mariupol na kiwanda cha chuma cha Azovstal, ambacho kipo chini ya udhibiti wa Urusi tangu miezi ya mwanzo ya vita.

Wizara ya Ulinzi Urusi imesema Askari wake waliokuwa wakishikiliwa na Ukraine wameachiliwa baada ya mchakato wa mazungumzo.

Ikumbukwe tu Urusi na Ukraine mara kadhaa zimekuwa zikibadilishana wafungwa wa kivita tangu mwanzoni mwa uvamizi wa Urusi mnamo Februari 2022, ikiwa ni mfano wa nadra wa mawasiliano ya bayana baina ya Mahasimu hao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags