Ujumbe wa K2ga wazua gumzo

Ujumbe wa K2ga wazua gumzo

Alooooh! Haya ni marangi marangi kama msanii mwenyewe alivyoimba katika wimbo wake alioachia siku chache zilizopita. Huyu si mwingine, ni yule mwamba anayecheza vyema na sauti yake kuleta ladha katika muziki wake maarufu kwa jina la K2ga kutoka label ya Kings Music baada ya kuandika ujumbe uliozua gumzo kwa mashabiki.

Msanii huyo amekuwa akifananishwa uimbaji wake na msanii mkongwe katika game ambaye pia ni boss wake Alikiba.

Kupitia ukurasa wa Instagram, K2ga ameandika ujumbe ambao umezua gumzo kwa mashabiki na baadhi kubaki na maswali kwamba msanii huyo anaondoka chini ya uongozi wa Alikiba au laah!, ujumbe huo ukisema,

“Usiwe na furaha sana unapoona watu wanakupenda na kukujali ni swali la kujiuliza ni je watakupenda mpaka lini? kwa sababu binadamu anabadilika muda wowote."

Dondosha comment yako hapo chini, je huo ujumbe kutoka kwa msanii huyo amemaanisha nini?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags