Tyla asimama na Chidimma Adetshina

Tyla asimama na Chidimma Adetshina

Mwanamuziki wa Afrika Kusini, Tyla amemamua kusimama na kumtetea mwanamitindo Chidinma Adetshina ambaye alijiondoa kwenye mashindano ya kuwania taji la Miss Afrika Kusini kufuatiwa na kubaguliwa kwenye shindano hilo, kwa madai ya kuwa ni raia wa Nigeria.

Mwanamuziki huyo anayetamba na ngoma yake ya ‘Water’ kupitia ukurasa wake wa X ametoa maoni kuhusu mwanadada huyo kuwa alichotendewa sio haki, huku akimtakia kila la kheri katika uamuzi wake aliouchukua.

Aidha kufuatia na maoni yake baadhi ya wananchi wa Afrika Kusini walimkosoa mwanamuziki huyo kwa kumuungua mkono Chidimma huku baadhi yao wakitoa maoni kuwa Tyla alipaswa kukaa kimya kuhusu suala hilo kwani maoni yake yanaweza kudhuru kazi yake.

Mshiriki huyo wa Miss Afrika Kusini 2024, Chidimma Adetshina (23) alijiondoa kwenye mashindano hayo Agosti 8, mwaka huu, huku akiweka wazi kuwa amefanya hivyo kwa ajili ya usalama wake na wa familia yake.

Utakumbuka kuwa siku chache zilizopita mitandao ya kijamii ya Afrika Kusini ilizua mijadala kuwa mmoja wa washiriki katika mashindano hayo siyo mtu wa taifa hilo wakidai kuwa ni Mnigeria huku wakihofia mrembo huyo kuwa huenda akaibuka mshindi kwenye fainali ya Miss SA zinazotarajia kufanyika Agosti 10, 2024.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags