Tyla aendelea kukimbiza Spotify

Tyla aendelea kukimbiza Spotify

Mwanamuziki wa Africa Kusini, Tyla ambaye alijulikana zaidi kupitia wimbo wake wa ‘Water’ ameendelea kufanya vizuri kupitia ngoma zake, hii ni baada ya albumu yake iitwayo ‘Tyla’ kufikisha zaidi ya wasikilizaji 1 bilioni katika mtandao wa Spotify.

Albumu hiyo yenye ngoma 14 ndani yake akiwa amewashirikisha wasanii Gunna, Tems, Travis Scott na wengineo, iliachiwa rasmi Machi 22, 2024 huku ikichukua miezi miwili tu kufikisha wasikilizaji bilioni 1.

Hayo siyo mafanikio ya kwanza kwa albumu hiyo kwani imewahi kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya ‘Billboard World Album Chart’ wiki chache tangu kuachiwa kwake na kuifanya kuwa album ya pili kwa mwanamuziki wa Africa kushika namba moja Billboard, huku ya kwanza ikiwa ya Wizkid iitwayo ‘Made in Logos’.

Hata hivyo mafanikio mengine ya msanii huyo yalionekana mapema mwaka huu baada ya kunyakuwa tuzo ya Grammy katika kipengele cha ‘Best African Music Performance’ na sasa ametajwa kuwania tuzo za BET 2024 ambazo zinatarajiwa kutolewa Julai 1 mwaka huu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post