Tetemeko jipya la Ardhi Uturuki na Syria watu wanasa kwenye vifusi

Tetemeko jipya la Ardhi Uturuki na Syria watu wanasa kwenye vifusi

Matetemeko ya ukubwa wa 6.4 na 5.8 yalipiga kusini mashariki karibu na mpaka na Syria, ambapo matetemeko hayo yaliharibu nchi zote mbili mnamo 6 Februari.

Kwa mara nyingine tena waokoaji wanatafuta watu waliokwama chini ya vifusi baada ya matetemeko mawili mapya ya ardhi kuikumba Uturuki na kuua takribani watu watatu.

Matetemeko ya awali yalisababisha vifo vya watu 44,000 nchini Uturuki na Syria huku makumi ya maelfu ya wengine wakiachwa bila makazi.

Shirika la maafa na dharura la Uturuki linasema tetemeko hilo la 6.4 lilitokea saa 20:04 saa za ndani (17:04 GMT), na kufuatiwa na tetemeko la 5.8 dakika tatu baadaye.

Vifo hivyo vitatu vilitokea Antakya, Defne na Samandag, Waziri wa Mambo ya Ndani Süleyman Soylu aliwataka watu kutoingia kwenye majengo yanayoweza kuwa hatari kwa usalama wao.

Soylu aliongezea kwa kusema kuwa watu 213 wamejeruhiwa kufuatia tetemeko hilo.

"Nilidhani dunia imepasuka chini ya miguu yangu," mkazi wa eneo hilo Muna al-Omar aliliambia shirika la habari la Reuters, huku akilia akiwa amemshika mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka saba.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags