Tatu bora wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani

Tatu bora wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani


Michezo inaonekana kuendelea kuwanufaisha watu waliojikita kwenye tasnia hiyo. Katika kulithibitisha hilo jarida la Forbes limetoa orodha ya wanamichezo wanaolipwa zaidi duniani

1, Cristiano Ronaldo – Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 39 mapato yake ya jumla ni $260 milioni (Sh 673 bilioni), mshahara wake wa kila mwaka ni $ 200 milioni(Sh 518.6 bilioni) kwenye klabu ya Al Nassr anayoichezea.

$60 Milioni (TSh 155.58 bilioni) anazipata kutoka kwenye mikataba mbalimbali nje ya uwanja. Mbali na mkataba wa maisha na Nike, Ronaldo anatengeneza pesa kwa mavazi yake yenye chapa ya CR7, vifaa, hoteli na ukumbi wa michezo.

2, Jon Rahm – raia wa Spain mcheza golf mwenye umri wa miaka 29 mapato yake ya jumla ni $218 milioni (Sh 565.27 bilioni). Mshahara wake ni $198 milioni (513.32 bilioni.) na $20 milioni anazipata kutoka kwenye mikataba mbalimbali.

Mafanikio yake yameonekana zaidi baada ya kujiunga na LIV Golf Desemba mwaka jana. LIV Golf ni mfululizo wa mashindano ya gofu yaliyoanzishwa mwaka 2021, yanayofadhiliwa na Saudi Arabia kupitia mfuko wa uwekezaji wa umma wa nchi hiyo (Public Investment Fund - PIF).

3, Lionel Messi raia wa Argentina na mchezaji wa klabu ya Inter Miami. Mapato yake ya jumla ni $135milioni (Sh 350.7bilioni), mshahara wake $65 milioni (Sh 168.8) pesa zitokanazo na madili nje ya uwanja ni $70 milioni(Sh 181,8).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags