Tajiri Murdoch kuoa tena kwa mara ya tano

Tajiri Murdoch kuoa tena kwa mara ya tano

Mwanzilishi wa vyombo vya habari na tajiri maarufu kutoka nchini Marekani Rupert Murdoch (92) anatarajia kufunga ndoa yake ya tano na mpenzi wake Elena Zhukova (67).

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo vimeweka wazi kuwa, ndoa hiyo itafanyika katika shamba la zabibu la Murdoch ambapo mpaka kufikia sasa bado haijawekwa wazi siku wala mwezi wa kufungwa kwa ndoa hiyo.

Hii inakuwa ndoa ya tano kwa tajiri Murdoch, ndoa yake ya nne na aliyekuwa mkewe Jerry Hall ilitamatika kwa kupeana talaka mwaka 2022 baada ya kudumu kwa miaka sita.

Rupert Murdoch ni tajiri namba 71 duniani ambaye anamiliki vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo Sky, Fox, Fox Entertainment Group, Sky Italia na vinginevyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags