Staa wa Man United atembelea Mikumi, Visiwa Vya Karafuu Zanzibar

Staa wa Man United atembelea Mikumi, Visiwa Vya Karafuu Zanzibar

Tanzania imeendelea kuwa kivutio cha watalii kuja kupumzika na kutembelea vituo vilivyopo, hii ni baada ya kiungo wa Manchester United na timu ya taifa Morocco, Sofyan Amrabat kuchapisha video akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo Morogoro.

Amrabat amechapisha video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa Mikumi na kusindikiza na ujumbe uliosomeka, “Pale Simba wa Atlas (jina la utani la nchi yake) akikkutana na Simba mnyama!”

Aidha, kiungo huyo awali alikuwa ametembelea visiwa vya Karafuu Zanzibar kabla ya kwenda Mikumi.



Staa huyo anaungana na mastaa wengine ambao wamekuwa wakitembelea Tanzania kipindi cha ligi zinapoisha na kuja kutali akiwemo beki wa mabingwa wa soka wa Ufaransa PSG, Ashraf Hakimi aliyepo pia Tanzania kwa mapumziko.

Amrabat amekuwa sehemu ya mafanikio ya United msimu uliopita wakichukua Ubingwa wa FA mbele ya Manchester City na kujihakikishia nafasi ya kucheza mashindano ya Europa msimu ujao baada ya kumaliza nafasi ya 8 na pointi 60.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags