Snoop Dogg ataja ma-rapa watatu anaowakubali

Snoop Dogg ataja ma-rapa watatu anaowakubali

Msanii nguli wa muziki wa hiphop kutoka Marekani, Calvin Cordozar “Snoop Dogg amewataja ma-rapa anaowakubali muda wote akiwemo Ice Cube.

Snoop ameachia listi hiyo ya mastaa wa muda wote kupitia mahojiano yake na mtangazaji Jimmy Kimmel, baada ya kuambiwa ataje wasanii wa Hip hop wa muda wote ndipo akamtaja Slick Rick, Ice Cube nay eye mwenyewe.

Alijibu “Slick Rick, Ice Cube na Snoop Dogg.”

List hiyo ya Snopp imeleta mapokeo tofauti kwa mashabiki kwenye mitandao ya kijamii huku wengi wao wakihoji kwanini hajawataja ma-rapa wakubwa kama 2PAC, Notorious BIG, Jay-Z na Eminem.

“Snoop nimiongoni mwa wasanii ambao waliwahi kufanya kazi kwa ukaribu na rapa 2pac enzi za za uhai wake kiasi chakuwa washikaji kwakuwa walikuwa wanatoka Record Lebo moja, licha ya hayo yote haijamfanya Snoop kumtaja 2pac kwenye list ya ma-rapa wake bora wa muda wote” Alihoji moja ya shabiki katika upande wa komenti






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags