Snoop Dogg amkumbuka Malikia Elizabeth

Snoop Dogg amkumbuka Malikia Elizabeth

Mwanamuziki kutoka Marekani Snoop Dogg amekumbuka mchango wa marehemu Malikia Elizabeth kutokana na mambo aliyowahi kumfanyia enzi za uhai wake.

Wakati alipokuwa kwenye mahojiano yake na ‘Capital FM’ Snoop aliweka wazi kuwa Malikia alikuwa shabiki yake sana na ndio maana alifanikisha msanii huyo asifukunze nchini Uingereza.

Utakumbuka kuwa mwaka 1993 Snoop alishitakiwa kwa mauaji na kufutiwa mashitaka hayo mwaka 1996 baada ya kutokuwa na hatia huku Malikia akizuia ‘rapa’ huyo asifukuzwa Uingereza wakati alipokwenda nchini humo kwa ajili ya ziara yake.

Kufuatia na mahojiano yake aliyowahi kuyafanya mwaka 2015 aliweka wazi kuwa Malikia alimtetea asifukuzwe kutokana na wajukuu zake kukubali ngoma zake.

“Walipojaribu kunifukuza kutoka Uingereza, Malikia alitoa maoni kwamba wajukuu zake walimpenda Snoop Doggy na hakufanya kosa nchini Uingereza, kwa hivyo alinipa ruhusa ya kuwa nchini hapo muda wowote”

Malikia Elizabeth II alifariki mwaka 2022 akiwa na umri wa miaka 96, kwa mujibu wa BBC Malikia alifariki kwa Amani nyumbani kwake Balmoral.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags