Ikiwa zimepita siku chache tu tangu kuweka rekodi kupitia onyesho lake la ‘Super Bowl Halftime’, ambalo limekuwa tamasha lililotazamwa zaidi katika historia, na sasa inaelezwa kuwa show hiyo imeendelea kumletea mafanikio makubwa Kendrick Lamar.
Gwiji huyo wa Compton ameweka historia rasmi kwa mara nyingine, akiwa msanii wa kwanza wa rap kuwahi kuwa na albamu tatu kwa wakati mmoja katika nafasi 10 za juu kwenye chati ya Billboard 200.
Kwa mujibu wa chati hizo Albamu mpya ya Lamar, GNX, imepanda hadi nafasi ya kwanza baada ya kuwa nafasi ya nne kwa muda mrefu huku ikiingiza mauzo ya juu zaidi tangu kutolewa kwake Desemba 2024.
Lakini pia albamu zake za zamani DAMN: Good Kid na M.A.A.D City zimerudi kwenye 10 Bora, zikisonga kutoka nafasi ya 29 na 27 hadi nafasi ya 9 na 10, katika chati ya Billboard 200.
Mbali na kupata mafanikio hayo lakini pia kupitia show hiyo amefanikiwa kuivunja rekodi ya marehemu mfalme wa pop Michael Jackson ambapo alipata watazamaji zaidi ya milioni 133.5 katika tamasha hilo na kumpikuwa MJ ambaye alifanikiwa kupata watazamaji milioni 133.5 ndani ya siku mbili.

Leave a Reply