Shangazi wa Nandy "Rich Aunty" awa gumzo mitandaoni

Shangazi wa Nandy "Rich Aunty" awa gumzo mitandaoni

Uwiiiiiiii! Wakati wewe ukivimba na kutamba kuwa una Shangazi bora basi wengine wako kimya na marich Anty wao chezea wewe, basi bwana inaonekana week hii ni week ya Nandile tuu nyie wengine subirini next week hahaha!.

Basi bwana kwenye gumzo mitandaoni imeonekana bado ile harusi ya kifahari iliofanyika pale Milimani City ya mwanadada Nandy imekuwa ndo stori ya mjini baada ya Shangazi huyo kumwaga Dollar kwa maharusi hao.

Aidha bibi Harusi huyo alifunguka na kueleza kiasi ambacho Shangazi alichomtunza na kueleza kuwa “ pesa alizo nitunza rich Anty  ni US  Dollar 12,000 ambazo ni sawa na Million 27.6 za Kitanzania” Amesema Nandy

Nandy aliendelea kufunguka kuhusiana na maoni mengi ya watu kupitia mitandao mbalimbali wakiuliza rich Anty bado yupo au ameondoka, basi bwana bibi harusi huyo akasema kuwa “ Shangazi bado yupo sana mana amesema anataka kunisindikiza katika show yangu ya Nandy Festival, Shangazi bado anataka kuendelea kunitunza yaani bado yupo sana” Amesema Nandy

Alooooh! Wanasemaga Shangazi ni Baba sasa hapa ndo naamini au vipi mdau wa Mwananchi Scoop wewe unashangazi au Rich Anty, dondosha komenti yako hapo chini mtu wangu wa nguvu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags