Shamsa Ford: Ishi maisha yako

Shamsa Ford: Ishi maisha yako


Aisee kutoka moja kwa moja kwenye ukurasa wa Instagram wa Muigizaji Shamsa Ford Kwenye ameachia ujumbe huu mzito akiwasihi watu kuishi kwenye uhalisia wao.

 ''Hakuna kitu kizuri kama kuishi kwenye uhalisia wako na uwezo wako usilazimishe kutaka sifa kwa watu huku unaumia mwenyewe.Naomba nikujuze mimi nilikaa miaka 2 bila kuwa na gari baada ya kuuza gari yangu pendwa kutokana na changamoto za maisha.Usafiri wangu ulikuwa ni Tax,bajaji na wala sikusononeka kwasababu ndo maisha yalitaka hivyo na sikutaka kulazimisha kwa kukodi magari kisa tu najulikana .

Niliyabeba matatizo yangu na kupambana nayo mwenyewe.Kuna siku nilikuwa kwenye bajaji na mwanangu akaniambia mama utapata gari kama ile hakuishia hapo siku nyingine tulikuwa mlimani city akaniambia mama tupige picture kwenye gari hii utapata,siku nyingine nilimsikia akisali akasema Mungu mpe gari mama yangu

.Mungu alinisaidia nikapata hii gari naithamini sana .Inaweza ikawa si gari ya thamani kwa wengine but ni nguvu yangu na inanisaidia.
Jifunze kutolazimisha kumiliki vitu vikubwa kama huna uwezo navyo pia jifunze kutofananisha maisha yako na mtu mwingine utaishi kwa Amani.

Naitamani prado new modern au jeep inshaallah ila mpaka tumalize zile issue mwanangu''.

Yes kwa ujumbe huo unampa asilimia ngapi Shamsa Ford? Dondosha comment yako hapo chini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags