Serikali ya Taliban yazuia wanawake kusoma vyuo vikuu

Serikali ya Taliban yazuia wanawake kusoma vyuo vikuu

Serikali ya Taliban imewazuia wanawake kutokusoma elimu ya chuo kikuu. Msemaji wa Wizara ya Elimu ya Juu amesema uamuzi huo ulifanywa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri na agizo litaanza kutekelezwa mara moja.

Hii ni hatua ya pili baada ya Machi 2022 Serikali kuzuia Watoto wa Kike kurejea Mashuleni pamoja na kuzifunga Shule zote za Wasichana muda mfupi baada ya kufunguliwa.

Aidha utawala mpya umelalamikiwa kukandamiza haki za wanawake na Wasichana tangu kuchukua Mamlaka Agosti 2021 na kuzuia Wanawake kushiriki katika shughuli nyingi za Kimaendeleo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post