Sababu zinazokufanya uwe jinsi ulivyo

Sababu zinazokufanya uwe jinsi ulivyo

Ni wakati mwingine tena tunakutana kupitia dondoo za saikolojia zinazokujia katika jarida letu la Instascoop na leo tumekuletea sababu zinazokufanya uwe jinsi ulivyo.

Tunafahamu kuwa tabia tulizanazo leo ni zile ambazo tumejifunza tangia tukiwa watoto na ndio zimetufanya tuwe hivi tulivyo.

Licha ya kwamba katika mambo ya saikolojia tunajifunza nafasi ya kuzaliwa inachangia kujenga au kubomoa maisha yako ila leo tutaangalia sababu zinazokufanya uwe jinsi ulivyo katika mahusiano.

Katika familia zetu kila mtu ana nafasi yake kama mtoto, maana yake ni kwamba kuna mtoto wa kwanza, kati, wa mwisho na mtoto wa pekee.

Kawaida ni kwamba mtoto anapozaliwa, kuanza kukua na anapokuwa mtu mzima, ni lazima kuna tabia zitaonekana na hata zingine kukua nazo.

Na tabia hizi mara nyingi zinaweza kuwa ni za asili, za kurithi, za kujifunza kutokana na mazingira ama nafasi aliyonayo na pia kuna zile za kufundishwa. Zoote hizi ni tabia ambazo zipo kati ya zile ulizonazo.

Leo tuangalie tabia ambazo ni za asili zitokanazo na nafasi ya kuzaliwa ya mtoto katika famili, kama nilivyosema hapo juu kuwa kuna makundi makuu matatu ya nafasi ya kuzaliwa katika familia.

Tabia hizi zinatafsirika vizuri kisaikolojia ingawa unaweza kukutana pia tabia hizi huingiliana kutegemeana.

Mtoto wa kwanza

Hawa ni watoto ambao huonekana kama neema na mwanga katika familia zao, malezi wanayoyapata ya upendo wa juu kutoka kwa wazazi huwafanya kuonekana wa pekee za zaidi.

Kwa mtazamo wa kiuhalisia na wa kisaikolojia watoto wa kwanza huwa na tabia kama hizi, hujiamini na kuaminika sana katika familia. Lakini hukosa kujiamini kwa haraka pindi anapopatikana mtoto wa pili.

Ni watoto ambao ni waangalifu sana na wapo makini lakini inapotokea kuharibikiwa, huaribikiwa kweli na huchukua muda sana kurudi kwenye hali ya kawaida hasa kurudisha uaminifu uliopotea.

Pia ni watu wanaoweza kupata mafanikio kwa haraka kutokana na nafasi waliyonayo katika familia kama kichwa cha familia. Na mara nyingi huisi ni wajibu wao kutake care of the family.

Vile vile wanaoweza kudhibiti na kujidhibiti hasa wanapokutana na hali ambazo huleta ugumu kwao, lakini inapotokea kukata tamaa hukata kweli.

Ni watu wenye hasira sana na za haraka, lakini mara nyingi hushindwa kutoa maamuzi ya haraka pale panapohitaji maamuzi pia wanapenda na kutaka kuonekana ni best kwa kila kitu ili kumaintain nafasi yao kama kichwa cha familia.

Lakini pia ni watu wanaopenda sana kampani au urafiki na watu wanaowazidi umri ama wadogo zaidi yao,mara nyingi hawapendi kuwa na marafiki au kampani ya watu wa umri unaoendana.

Katika mahusiano na ndoa

Katika mahusiano ya ndoa mtoto wa kwanza anataka kumtawala kila mmoja ambaye yupo chini yake ili nafasi yake ya kuzaliwa iweze kuoneka kwamba yeye anatawala kutokana na tabia nilizoelezea hapo juu.

Hapo sasa ndoa lazima itakuwa na shida hasa kama aliyeolewa kwenye hiyo familia   naye ni mtoto wa kwanza alikotoka. ndugu watasema anamkali kaka yetu kumbe ni ile tabia ambazo ziko katika nafasi yake ya kuzaliwa.

Nini ufanye

Ukisha kujua mtu unayeishi naya ni mzaliwa kwa kwanza anza taratibu kuongea naye mpe ukweli wa tabia ambazo nimeziandika hapo juu kwamba ni lazima akubali kubadilika tabia zake ili muweze kwenda pamoja.

Katika kubalika hawezi kubalika kwa haraka anahitaji muda kwa sababu saikolojia yake, hisia zake, na hata katika kimwili hizo tabia tayari zimejengeka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post