Kendrick Lamar Kuungana Na Sza Kwenye Super Bowl

Kendrick Lamar Kuungana Na Sza Kwenye Super Bowl

Nyota anayetamba na ngoma ya ‘Not Like Us’ Kendrick Lamar ambaye atatumbuiza katika onyesho la Halftime la Super Bowl ameripotiwa kuwa hatofanya show hiyo mwenyewe bali ataungana na SZA.

Taarifa hiyo imetolewa na jukwaa la ‘Apple Music’ ikionesha kuwa watakuwa pamoja kwenye onesho hilo. Ushirikiano wa wawili hao sio tu wote ni wasanii na wanaupiga mwingi kupiti ngoma zao lakini pia wamewahi kuachia ngoma nyingi za pamoja ikiwemo Luther, Gloria na nyinginezo.

Ikumbukwe uteuzi huo wa Lamar kukiwasha kwenye Super Bowl ulileta mkanganyiko kupitia mitandao ya kijamii watu wengi kudhani msanii ambaye anafaa ni Lil Wayne ambaye ni mzaliwa wa New Orleans.

Wasanii wengine waliowahi kupata nafasi ya kuonesha ujuzi wao katika onyesho la Halftime la Super Bowl ni pamoja na Usher, The Weeknd, Lady Gaga, pamoja na icons kama Michael Jackson na Prince. Huku 2025 ikifanyika Februari 9 jijini New Orleans






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags