Ruger: Watanzania nimefika na mabegi yangu

Ruger: Watanzania nimefika na mabegi yangu

Niaje wanangu wa faida? Manake hapo kwanza nicheke, 'asiyefunzwa na mamae atafunzwa na ulimwengu,' sio maneno yangu hayo ni maneno ya waswahili na hao walimwengu sasa ni Watanzania.

Aloooh! Baada ya sakata la msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria mzee wa Buga maarufu Kizz daniel kutua Bongo kwa lengo la kutumbuiza miezi kadhaa iliyopita lakini alishindwa kufanya show hiyo kutokana na mabegi yake ya nguo kusahaulika kwenye ndege.

Basi bhana staa wa muzikii kutoka hukohuko Nigeria maarufu kwa jina la Ruger akasema ya nini mie yanikute kama aliyomtokea mzee wa buga,kwa ambao hawamfahamu mwana  ndo yule makalii aliyeachia hit songs  ndani ya kipindi kifupi  na moja ya ngoma zilizomtambulisha kwa mashabiki ulimwenguni ni wimbo wa  Bounce, Dior.

Kupitia ukurasa wa Twitter Ruger ameandika ujumbe ukisema  watanzania nimefika bila kusahau mabegi yangu, tukutane tarehe 1 october.

"Tanzania!! I’m here and i didn’t forget my bags .See you October 1st."

Msanii huyo ambaye kwasasa yupo Tanzania akijiandaa kwa ajiri ya show itakayofanyika tarehe 1 october,bongo hatuna mbambamba tunataka mziki mzuri hapa kazi kazi.



 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags