Rostam adhamiria kuwekeza Zambia

Rostam adhamiria kuwekeza Zambia

Mfanyabiashara kutoka Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla Rostam Azizi, ametangaza uwekezaji mkubwa katika gesi ya Liquefied Petroleum Gas (LPG) nchini Zambia, ambao utakuwa mradi wa kwanza wa (LPG) nchini humo.

Bilionea huyo alitangaza uwekezaji huo utakaofanywa na kampuni yake ya Taifa Gas, amesema inawekeza katika sekta ya umeme nchini Zambia kupitia ubia na kampuni ya ndani ya Zambia, Delta Marimba Limited.

Kiwanda cha kuzalisha umeme, kitakapoanza kufanya kazi, kitachangia ziada ya megawati 100 za nishati thabiti kwenye gridi ya taifa ya Zambia.

“Tanzania na Zambia zina uhusiano mkubwa wa kihistoria, na haijawahi kuwa na fursa nzuri zaidi ya kuwekeza nchini Zambia tunafuraha kuchangia katika mazingira ya nishati ya Zambia na kukuza uhusiano wa karibu kati ya Tanzania na Zambia.”alisema Bilionea huyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags