Rihanna apotezea mashtaka dhidi ya baba yake

Rihanna apotezea mashtaka dhidi ya baba yake

Ebwana eeh nikwambie tu kilichojiri kutoka kwa muimbaji na muigizaji Rihanna bwana ameripotiwa kuachilia mashtaka dhidi ya baba yake mzazi, Rondald Fenty juu ya madai ya kutumia jina la familia ‘Fenty’ na umaarufu wa mtoto wake kujiingizia kipato kinyume na Sheria.

Aidha kama ilivyoripotiwa hapo awali mwimbaji huyo alifungua kesi dhidi ya baba yake 2019 na walipaswa kufika mahakamani mwezi huu juu ya suala hilo, ambapo Rihanna alitaka baba yake kulipa fidia pamoja na kuitaka mahakama kusimamisha shughuli za kampuni hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 2017.

Imeelezwa kuwa baba mzazi wa star huyo alishirikiana na mfanyabiashara mwenza Moses Perkins kuanzisha kampuni yao, Fenty Entertiment ambapo wamekuwa wakifanya kazi za uwakala wa Rihanna kwa kutafuta shows na kupiga Mkwanja mrefu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags