Rayvanny atoa shukrani kwa mastaa Paris

Rayvanny atoa shukrani kwa mastaa Paris

Akiwa anaendelea na ziara yake kwa ajili ya kufanya kazi na wasanii mbalimbali, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Rayvanny ametoa shukurani zake za dhati kwa wasanii kutoka katika mataifa mbalimbali kwa kujumuika naye studio kuandaa nyimbo.

#Rayvany kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share ujumbe wa kutoa shukrani kwa vyombo vya habari nchini Ufaransa pamoja na wasanii huku akidai kuwa jina lake kwasasa lina heshima ya level nyingine kutokana na alivyopokelewa na baadhi ya mastaa jijini Paris.

Kwa sasa mwanamuziki huyo yupo jijini Paris nchini Ufaransa kwa ajili ya kufanya kazi na ‘mastaa’ mbalimbali nchini humo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags