Rappa Lanez jela miaka 13

Rappa Lanez jela miaka 13

Rapa kutoka nchini Canada Tory Lanez amekutwa na hatia ya mashtaka matatu ya uhalifu kwa kumpiga risasi Megan Thee Stallion, waendesha mashtaka wamependekeza kifungo cha miaka 13 jela kwa msanii huyo.

Alhamisi, Juni 1 wakili Matthew Barhoma, kwa niaba ya Tory Lanez, aliwasilisha ombi la kuahirisha hukumu ya rappa huyo huko California.

Hati ya hukumu iliyopatikana Jumanne (Juni 6), iligusia habari potofu za Tory kupitia muziki na machapisho yake kupitia mitandao ya kijamii ambayo inaeleza yalisababisha madhara ya kisaikolojia kwa Megan.

Hati hiyo pia imeelezea shambulio la Lanez dhidi ya August Alsina, ambalo lilitokea backstage katika tamasha la vichekesho huko Chicago mwezi Septemba mwaka uliopita.

Mawakili wa mashtaka hapo awali walitaka adhabu kali itolewe kwa msanii huyo kutokana na kuonesha ukatili mkubwa na kutojali kabisa maisha ya binadamu baada ya kudaiwa kumpiga risasi Megan mguuni wakati wa mzozo uliosababishwa na ulevi mwezi Julai 2020.

Aidha mawakili Matthew Barhoma, pamoja na Jose Baez walio upande wa Lanez, walidai kuwa Jaji Herriford alionesha upendeleo katika kesi hiyo ingawa bado hakuna uamuzi kutoka Mahakama ya rufaa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags