Rapa chipukizi Stylee( NIT)

Rapa chipukizi Stylee( NIT)

It’s  Friday bhana kama kawaida siku hii huwa tunaruka na zile makala zote za michezo na burudani hususani kwa wasanii chipukizi kutoka vyuo mbalimbali hapa nchini.

Wiki hii bhana nakuletea kijana chipukizi kwenye sanaa mkali wa hizi kazi bwana, kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) hapa nikizungumzia mtu mbadi Daniel Isaya maarufu kama  Stylee.

Kijana huyu bwana anajihusisha na uimbaji wa muziki wa kizazi kipya lakini anatembea kwenye zile ladha konkiii wenyewe wanaita Hip Hop yaani style flanii hivi za kufoka fokaa.

Akizungumza na Mwananchi Scoop, Stylee anasema ukiachana na masomo anayosoma muziki ni kama alternative yake kwa upande mwingine wa shilingi bhana.

Yote hayo anafanya akiwa anachukua  course ya Business Information Technology yaani (BIT), mwaka wa tatu.

Stylee amesema ameamua kujikita kwenye muziki kwasababu anaikubali sana sanaa na iko ndani ya moyo wake.

Vilevile amesema kuwa anaikubali sana Hip Hop kutokana na namna inavyowasilishwa kwa jamii, kwani iko tofauti na mitindo mingine na anavutiwa nayo sana kwasababu haumpi changamoto kuufanya.

Hata hivyo ameelezea soko la muziki wa bongo flavor  na kubainisha kuwa now days umepiga hatua sio kama zamani kwani hata ukitazama East Afrika wanaongoza.

“kwa sasa hivi tumetoboa sana kwanza kwa East Africa hakuna nchi ambayo mziki wake unaongoza kama Tanzania hata ukiangalia nyimbo zinazo trendi ukienda Kenya unakuta mtu wa kwanza hadi wa tano anatoka nyumbani” anasema na kuongeza

“halkadhalika Uganda hivyo hivyo kwahiyo  kibongo bongo sasa hivi Afrika na East Afrika kwa ujumla  tumeenda mbali sana hata wasanii ukiangalia top ten Afrika huwezi kukosa wabongo wawili au watatu” anasema.

Aidha ukiachana na sanaa Stylee anajihusisha na mpira wa miguu pamoja na sweeming ni vitu ambayo anavipenda pia.

Hata hivyo ametoa ushauri wake kwa vijana wote ambao wanachipukia kwenye sanaa akiwataka wawe na umoja yaani waweze kusurpotiana katika kazi zao ambazo wanazifanya kwani kufanya hivyo wanaweza kufika mbali kwenye kazi zao.

“Unakuta mtu unachukua muda mwingi sana kumsupoti msanii mkubwa kwa kushare kazi zake na kumpigia kelele lakini ile juhudi tungeifanya kwenye kazi zetu sisi underground kiukweli tungeweza kuinuka kwa haraka kikubwa tuwe na umoja itatusaidia” anasema.

Vile vile stylee anamalengo makubwa kwenye sanaa anayoipigania kwani anasema kuwa Muziki ni ajira rasmi na nimkombozi kwa vijana wengi.

“Malengo yangu ni kufika mbali nije kuwa msanii mkubwa niweze kuisaidia familia yangu kwani muziki ni ajira,  ukiangalia sasa hivi ajira ni ngumu sana sana hivyo naamini kupitia muziki ninaweza kupata ajira yangu ya kudumu mwenyewe” anasema

Sambamba na hayo Stylee anasema moja ya changamoto ambazo wanapitia wakiwa kama underground ni masuala mazima ya capital yaani wakati wakuwasilisha nyimbo zao hukumbana na changamoto hiyo.

“Unakuta unataka kutoa audio yako au hata video balaa linakuja kwenye pesa, huna pesa ya kutosha yakuweza kufanya video yenye ubora hivyo unatafuta tu mshikaji ilimradi akusaidie kazi itoke lakini haina ubora unaohitaji” anasema.

Hata hivyo akizungumzia uhalisia wa course anayoichukua  amesema kuwa sio nyepesi kama watu wanavyofikiria kwani inahitaji kutuliza akili ili uweze kufanikiwa zaidi katika masomo.

Vile vile amesema inahitaji muda mwingi sana wa kujisomea jambo ambalo ukikosa kujipa muda, masomo yanaweza kukushinda na ukajikuta unachukia course yenyewe.

Huku sanaa huku kitabu unapambana vipi hapo?

“Huku sanaa huku kitabu, kitabu kinahitaji muda na sanaa pia vile vile kwahiyo hapa nafanya plan zote B na A nacheza 50 kwa 50 kwasababu zote ni ajira hizi lazima nizimbanie vile niwezavyo”anasema.

Ukiwa katika kazi zako za sanaa unapendelea kuvaa mavazi gani?

“Mara nyingi huwa navaa kulingana nasehemu siwezi kwenda studio hua napenda kuvaa kawaida lakini nikienda kwenye kushoot hua navaa nguo zangu za kazi, kama ni mambo ya fashion basi nitatoka kifashion yaani navaa kulingana na mazingira”anasema.

Kipi kipaumbule chako kwenye maisha yako?

“kwenye maisha bwana kuna wazazi ukiachana na wewe mwenyewe ambao ndiyo kama viongozi wa duniani hao wanaushauri wao wanaweza kukushauri hivyo wanaweza kukupa kipaumbele chao”anasema na kuongeza

“Mimi kama mimi kipaumbele change ni elimu hiyo ndiyo plan A yangu lakini plan B ninazo ikiwemo muziki, mpira wa miguu na masuala ya kuogelea”anasema.

Ayaaaa!!! Nikukwambie tu huyo ni Stylee ambaye ndiyo underground wetu wa leo kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji akisisitiza zaidi kuwa wasanii Chipukizi mnatakiwa kubebana kuwa wamoja na kusupotiana katika kazi zenu.

Nakupa fursa kupitia makala ya leo kama ni kijana na unakipaji basi tufollow kupitia ukurasa wetu wa Instagram@MwananchiScoop au unaweza kucomment hapo chini nasi tutaruka na weweee happy weekend bosss!!!!!!!!!!






Comments 3


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags