Ramaphosa akanusha kuipendelea Russia

Ramaphosa akanusha kuipendelea Russia

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameeleza kwamba msimamo wa nchi yake usio fungamana na upande wowote kuwa haufanyi upendeleo nchi ya Russia dhidi ya mataifa mengine na kusisitiza wito wake kusuluhisha mgogoro wa Ukraine kwa amani.

Taarifa hiyo ilijiri mara baada ya madai ya Marekani wiki ilio pita kwamba silaha zilipakiwa kwenye meli ya Kirusi Lady R, kutoka kambi ya wanamaji mjini Cape Town mwishoni mwa mwaka jana, ambayo yalizua mzozo wa kidiplomasia.

Sambamba na hayo aliongeza kwa kueleza kwamba Afrika Kusini itaendelea kuheshimu mikataba ya kimataifa ambayo imetia saini na mbinu yake ya kukabiliana na madai ya Marekani ya usafirishaji wa silaha itatii makubaliano hayo, aliongeza.

Aidha ofisi ya Raisi huyo imesema hakuna ushahidi madhubuti uliotolewa kuunga mkono madai yaliyotolewa na balozi huyo, lakini uchunguzi utakaoongozwa na jaji mstaafu, utaangazia madai hayo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags