Rais wa Marekani  aahidi kufanya ziara barani Afrika

Rais wa Marekani aahidi kufanya ziara barani Afrika

Rais wa Marekani Joe Biden ameahidi kufanya ziara barani Afrika, kusini mwa jangwa la Sahara ambayo itakuwa ya kwanza katika wadhifa wake wa urais.

Rais Biden atafanya ziara hiyo wakati ambapo China na Urusi zinaimarisha uhusiano wa kiuchumi na kijeshi na nchi za Afrika.

Kwenye mkutano na viongozi wa nchi kadhaa za Afrika mjini Washington mapema wiki hii Biden aliahidi vitega uchumi thamani ya dola bilioni 55 kwa nchi za Afrika katika sekta za biashara na kwa ajili ya misaada ya maendeleo.

 Kiongozi huyo wa Marekani pia amependekeza ushiriki wa kudumu wa Umoja wa Afrika kwenye vikao vya kundi la nchi 20 zinazoongoza kiuchumi duniani. Amesema Afrika inastahili kuwa na kiti kwenye kila sehemu.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post