Rais Volodymyr Zelensky kufanya ziara nchini Marekani

Rais Volodymyr Zelensky kufanya ziara nchini Marekani

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ametoa taarifa leo kuwa yuko safarini kuelekea nchini Marekani ambako atakutana kwa mazungumzo na Rais Joe Biden kwa lengo la kile alichosema ni kuimarisha ustahimilivu na ulinzi wa Ukraine.

Hii itakuwa ni ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi tangu Urusi ilipoivamia nchi yake Februari 24 mwaka huu. Katika ziara hiyo, Zelensky anatarajia pia kulihutubia Bunge la Marekani.

Bunge hilo linajiandaa kupiga kura ya kuridhia kitita cha dola bilioni 45 za msaada wa dharura kwa Ukraine lakini pia ikijiandaa kupeleka mfumo wa kujilinda angani wa Patriot ili kuisaidia kupambana na mashambulizi ya Urusi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags