Portable: Muziki unalipa kuliko mpira

Portable: Muziki unalipa kuliko mpira

Msanii kutoka Nigeria Habeeb Okikiola ‘Portable’ amefunguka kwa kudai kuwa muziki unalipa kuliko mpira wa miguu huku akishangazwa na wanaodai kuwa wachezaji mpira wanahela kuliko wasanii.

Portable ameyasema hayo kwenye moja ya video yake inayoendelea kusambaa kupitia mitandao wa kijamii akiamini kuwa wasanii wana nafasi kubwa ya kuwa matajiri kuliko wachezaji mpira.

“Pesa ambayo wasanii wanaipata kupitia muziki ni kubwa kuliko pesa ya soka, Wanamuziki hupata zaidi ya wapenda matambiko na walaghai. Mapato ya Apple Music ni makubwa, Wana-soka hawawezi kushindana, watu wanaosema wanasoka wanapata zaidi kuliko wanamuziki hawajui wanachosema. Wanamuziki wako kileleni”

Kauli hii huenda ikasadiki yaliyomo kwani kwa mujibu wa takwimu mbalimbali zinawataja wasanii kama, Taylor Swift, Jay Z na Rihanna kuwa mabilionea kufuatia na harakati zao za kimuziki lakini kwa wachezaji wa mpira wa miguu bado hawajafikia hatua za kuwa mabilionea licha ya kulipwa mpunga mrefu.

Portable anatamba na ngoma zake kama ‘Akoi Grace’, ‘The Germination of Sound’, ‘Bye To Sapa Nation’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags