Perfume 10 bora zinazopendwa na wanawake

Perfume 10 bora zinazopendwa na wanawake

Hellow! Jambo watu wangu wa nguvu, sasa leo bwana kwenye fashion nimekuja na jambo kuntu nikisema hivyo na maanisha, yaani wadada wengi wa siku hizi wanajipulizia tuu manukato. Kwanza inabidi ujue je haya manukato unayotaka kutumia yanakubali mwili wako au laaah!

Nazungumza hivi kwasababu kuna baadhi ya watu wakina dada hupenda manukato wanayotumia marafiki zao lakini wao wakitumia hawanukii kama wao, jua jasho lako na mwili wako unafaa manukato gani ndo ukanunue.

Sasa leo nimekusogezea orodha ya manukato ya wanawake ambayo ni updated kila msimu, najua kwa hizi nilizoandika huwezi kukosa ambayo inaendana na wewe.

  1. Guerlain La Petite Robe Noir

Waswahili wenyewe wanasema mwamba huyu hapaaa. Nikizungumza hivyo nadhani naeleweka kabisa yaani. Huu ni unyunyu classic ambayo hutumiwa na kupendelewa sana na baadhi ya watu wazito. Perfume hii bwana iko na ladha ya matunda, berry na mimea. 

  1. Milioni Lady, ya Paco Rabanne

Perfume nyingine ambayo hupendelewa na wanawake wengi kwakuwa na ladha ya harufu ya kumvuta mtu kwa jina linguine tusema ina harufu kali kidogo, ina ladha ya mchanganyiko wa asali na jimmy, kuna raspberry, hii ni jamii ya strawberry, pia iko ya machungwa nk.


  1. Afyuni, Yves Saint Laurent 

Wale wapenzi wa udii udii mwamba huyu hapa, sio poa maana ina harufu nyingi kama vile karafuu, mdalasini ubani, oud, vanilla, peach nk. Wewe dada mrembo unayependa kunukia unyunyu wa oud basi hii itakufaa.

  1. Versace Bright Crystal

Walee wazee na ndoa zao wapenda kufusha manukato ya miski, hii hapa nyingine ni nzuri mno na ukipulizia ndani mpaka mtaa wa saba wanasikia, wale wapenzi wa miski wananielewa nini namaanisha yaani harufu yake haikeri.

  1. Nina Ricci

Haya ni manukato bwana ambayo yamekaa kidada zaidi maana hata muuondo wake nje uko kirembo zaidi licha ya kuwa na harufu nzuri na hata ladha ya harufu yake imetawaliwa na maua zaidi.

  1. D & G 3 L'Imperatrice

Unyunyu huu bwana unamfanya mwanamke kujiamini haswa anapokuwa mbele za watu maana hata ladha za harufu yake ni ya kipekee sana kama vile unyunyu wa tikiti maji, miski nk yaani ukijipulizia lazima harufu yako ionekane ya tofauti mbele za watu.

  1. Green, DKNY

Haya ni manukato ambayo muundo wake kwa nje ni kama apple na maji yake kwa ndani like green apple ndo maana ikaitwa jina hilo na harufu nzuri mno maana manufacture iliotumika kutengenezea ni lile tunda alilokula Eva apple yaani perfume hii ni balaa. 

Mbali na kuwa na jina hilo la green likiwa na maana ya green apple pia katika kampuni hii kuna ladha za harufu mbalimbali kama vile tango, zaituni, rose nk.


  1. Armani Giorgio

Kuna baadhi wao hupendelea sana manukato ambayo yana harufu tofauti na mwingine, basi hili ndo suluhisho kwasababu Armani ina ladha ya harufu tofauti tofauti kama vile machungwa, limao, tangawizi nk, kama unahitaji harufu ya pekee yako basi nakushauri tumia hii kitu utakuja kunishukuru baadae.

  1. Givenchy Ange Ou Demon Le Secret

Wale wenzangu na mie wasiopenda harufu za karaha, tusiopenda mbambamba, unyunyu huu hapa wale wa lemon yenyewe wazee wa kupenda manukato ya maua basi hapa ndo kwisha kazi, uende kwengine ufuate nini. Hii nayo ni perfume ambayo hupendelewa sana kutumiwa na wanawake mbalimbali. 

  1. Gucci Guilty

 Uuuuwiiih! Wale wazee na vipenzi vya Gucci, sio unavaa nguo tu za kampuni hiyo halafu manukato yakushinde dada, nikuibie siri ya unyunyu huu bwana unakaa haswa kwenye nguo, kuna ladha za harufu tofauti tofauti kama vile chenza, limao, maua nk unakosaje kuitumia kwa mfano. 

Nyie nyie staki kuongea sana nifanye kama nimemaliza vile mtoto wa kike, mtoto wa mjini sharti ukipita sehemu nyuma watu waseme naam sio binti unanuka changamoto. Raha ya vitu vizuri uvigaramie, acha kutumia manukato ya bei rahisi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags