Vatican city Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis, amesema upo umuhimu mkubwa kwa sasa kuufanyia mabadiliko Umoja wa Mataifa na hasa baada ya janga la uviko-19 na vita nchini Ukraine.
Hayo yamo katika muhtasari wa kitabu chake kilichochapishwa ii leo. Kiongozi huyo amesema uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine Februari mwaka huu, umedhihirisha haja ya kuhakikisha kuwa muundo wa sasa wa ushirikiano wa kimataifa, na hasa Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa, unapata njia nyepesi na zenye ufanisi za kutatua mizozo.
Papa Francis aidha amekosoa suala la kukosekana kwa usawa katika mgawanyo wa chanjo, akiufananisha na sheria ya mwenye nguvu kutawala dhidi ya mshikamano.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 85 ameshauri kufanyika kwa mageuzi hai, yanayolenga kuruhusu mashirika ya kimataifa kutambua upya madhumuni yake ya kutumikia wanadamu, na kusema taasisi za kimataifa zinapaswa kuwa mlango utakaosababisha makubaliano mapana.
Leave a Reply