Nyota ya Diddy ya Walk of Fame haitaondolewa

Nyota ya Diddy ya Walk of Fame haitaondolewa

Baada ya kuandamwa na kesi za unyanyasaji wa kingono huku baadhi ya makampuni aliyokuwa akishirikiana nayo yakivunja mikataba, sasa wadau mbalimbali wanataka nyota ya mkali wa Hip-hop Diddy ya ‘Hollywood Walk of Fame’ iondolewe kutokana na tuhuma zake.

Kwa mujibu wa Tmz iliwasiliana na msemaji wa Chama cha Wafanyakazi cha Hollywood ambaye ameeleza kuwa shirika hilo bado halijakaa na kujadili kuondolewa kwa nyota hiyo ya heshima.

Hata hivyo Tmz ilieleza kuwa shirika hilo lina haki ya kutengeneza, kuweka nyota, kufanya hafla ya utoaji wa ‘Walk of Fame’ lakini haina mamlaka ya kuondoa nyota ya muhusika, hivyo basi ukiachilia mbali Combs kuhusishwa katika kesi saba za unyanyasaji wa kingono na makosa mengine lakini nyota ya Diddy itaendelea kusalia katika jumba hilo.

Ikumbukwe kuwa Sean "Diddy" Combs alitunukiwa nyota hiyo ya heshima ya Hollywood Walk of Fame Mei 2, 2008.

Hollywood Walk of Fame ni nyota ya heshima inayopachikwa kando ya barabara za Hollywood Boulevard na Vine Street ambapo kila nyota ina jina la mtu mashuhuri ambaye ametoa mchango mkubwa katika tasnia ya burudani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags