Njombe wapigwa Marufuku kula kitimoto

Njombe wapigwa Marufuku kula kitimoto

Alooooooh! Wale wapenzi wa hii kitu kama nawaona mnavyo kwazika maana kuna baadhi ya watu hawawezi kulala bila kula nyama  ya kitimoto taarifa zilizo tufikia ni kwamba.

Halmashauri ya Wilaya ya Makete mkoani Njombe imepiga marufuku Watu kuchinja Nguruwe na kula nyama yake (kitimoto) kwa muda usiojulikana kutokana na taarifa za uwepo wa ugonjwa wa homa ya nguruwe.

Aidha Afisa Mifugo na Uvuvi wa Wilayani humo Aldo Mwapinga ametoa taarifa ya katazo hili kutokana na vifo vya nguruwe 21Afisa huyo amesema kuwa  "Kata ya Tandala kumeripotiwa dalili za ugonjwa wa homa ya Nguruwe kwahiyo tunaendelea na jitihada za kuhakikisha tunashirikiana na Watendaji kuanzia ngazi ya Kata hadi Vitongoji kutoa taarifa juu ya hali inavyoendelea” amesema Aldo Mwapinga

Aliendelea kwa kusema Serikali imepiga marufuku hiyo hususani katika kata ya Tandala huku pia akizuia utoaji wa Nguruwe kutoka kwenye zizi moja kwenda jingine kwa ajili ya kupandisha kwa jike, vilevile amewataka Watu kuacha kufukua Nguruwe waliofukiwa baada ya kufa (mizoga) na kuwachinja kisha kwenda kuuza nyama hizo vilabuni nyakati za usiku.

 

 

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags