Njia za kuondoa magaga

Njia za kuondoa magaga

Hellow its Friday tena guys this is fashion kama kawaida yetu bwana ndiyo sehemu pekee ya kujidai na kupambania urembo bila kusahau mionekano yetu.

Ebwana wiki hii tutaangazia jinsi ya kuondoa Magaga kwenye nyayo za miguu aiseee jamno hili sio geni kwako ni Dhahiri kuwa umeshawahi kumuona au kusikia mtu mwenye changamoto hii lakini je, vipi inatatuliwa?

Hapo ndo pakujiuliza maswali, ni rahisi tu kupitia dondoo ya fashion wiki hii basi majibu yote yako hapa karibu kwenye mbinu na njia mbadala za kuondoa magaga kwenye nyayo.

Magaga hutokana na ukavu wa ngozi, japo hayaumi na hayana madhara makubwa lakini ukiwa na magaga unapata tabu sana kuvaa viatu vya wazi kwa sababu ya aibu, hizi ni njia tatu za kuweza kuondoa magaga

kabla ya kwenda kulala scrub miguu yako kwa kufanya hivi

  • chemsha maji yawe ya uvugu vugu
  • mimina kwenye beseni
  • weka sabuni katika maji yako
  • na tumbukiza miguu kisha uanze kusugua kama na jiwe au brush
  • ukimaliza kausha miguu na kitambaa kikavu na upake mafuta kisha vaa socks ulale nazo usiku mzima
  • fanya hivi kila siku mpaka magaga yatakapo isha

MAJI YA LIMAO

  • kata limao vipande viwili
  • chukua kimoja na uanze ku sugua katika magaga yako hakikisha maji ya limao yana ingia au kupita katika magaga yako
  • fanya hivi kwa muda usio pungua dakika tano
  • kisha sugua magaga yako kwa brush/jiwe
  • na uoshe miguu yako

OLIVE OIL

  • paka mafuta ya olive katika pamba
  • anza kusugua katika magaga yako kwa mfumo wa duara kwa dk15-20
  • vaa socks na iache kwa lisaa limoja.


Alooooh !!! sijui umenielewa hapo ukifuata procedure zote hizo suala la magaga utalisikia tu kwa jirani maana wewe utakua ushapata ufumbuzi wa kina kabisa.

Nikukumbushe tu kwa content mbalimbali za fashion na urembo usikose kufutilia magazine yetu kila ijumaa lakini pia unaweza kutembea website yetu www.mwananchiscoop.co.tz ahsanteeee!!!!

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags