Nipe dili Makange ya nyama

Nipe dili Makange ya nyama

Hatarii weuwee!! Jikoni leo kwenye ukurasa wa Nipe Dili nakusogezea upishi wa Makange ya Nyama bhnaa mate hayoo, nadhani utamu wa makange kwa wale waliobahatika kula unafahamika haswaa usijali kuanzia utaweza kuandaa mwenye udambu udambu huu.

Karibu nikufahamishe mwanzo mwisho jinsi ya kupika makange ya nyama ambayo unaweza kula kwa chakula chochote kile ikiwemo ugali, wali au hata chapati za kusukuma unaweza kulia pia twende sawaaa!!.

Mahitaji

  • Nyama  kilo moja steki 
  • chunvi
  • Pilipili
  • limao
  • vitunguu  Maji
  • Karoti
  • Katakata  nyama  kwa vipande  virefu 

Bila shaka mahitaji utakuwa umeshafahamu hapo kilichobaki sasa ni kuingia jikoni kuandaa makange yetuu.

  • Hakikisha unaosha  vizuri nyama  yako  
  • Kwangua  tangawizi  moja  kisha  kamulia  maji  yake  katika  nyama  yako  
  • Chukua  Kitunguu saumu  kilichomenywa  twanga  kisha  uchanganye 
  • Chukua  limao  kipande  kamulia
  • Weka  na Pilipili  manga  kidogo  tu2  
  • Weka  na chumvi  kidogo  kisha  vichanganye  vizuri  viungo  vyako katika nyama  
  • Funika  pembeni  kwa  muda  wa  dakika  5
  • Ili  viungo  viingie  vizuri  kwenye  nyama 
  • Katakata  vitunguu  Maji  vipande  vidogo  vidogo 
  • Karoti  katakata  kwa  urefu  na hoho  pia  kwa  urefu 
  • Chukua  sufuria  kavu  weka  jikoni  weka  mafuta  ya kula  kiasi  cha kuivisha  Kitunguu 
  • Weka  nyama  yako  iache  ichemke  kwa  muda  kidogo  Maji Maji  yakianza  kukauka  weka  nyanya  ilio  sangwa  upendavyo 
  • Kisha  weka  Karoti  Zako  pamoja  na hoho  
  • Acha  kwa  dakika  mbili  au  tatu  
  • Makange  Yako  yatakuwa tayari  kwa  kuliwa
  • Unaweza kula kwa ugali, chapati au wali ama chochote utakachopenda kati ya hivyo nakutakia mapishi mazuriii enjoy ukiwa jikoniiiii .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags