Ngoma za wasanii wa Universal Music Group kuchezwa WhatsApp

Ngoma za wasanii wa Universal Music Group kuchezwa WhatsApp

Kampuni ya Meta inayojihusisha na mitandao ya kijamii pamoja na kampuni inayoongoza duniani kwa kutoa burudani ya muziki 'Universal Music Group (UMG)' zimeingia makubaliano mapya ya nyimbo za UMG kutumika kwenye WhatsApp kwa mara ya kwanza.

Kwa mujibu wa tovuti ya Universal Music Group (UMG) imeeleza kuwa kama walivyoingia mkataba na majukwaa mwengine ya Meta yakiwemo Facebook, Instagram, Messenger, Horizon, na Threads hivyo basi sasa wameamua kuweka burudani ya muziki kwenye WhatsApp ili kulinda haki za wasanii na waandishi.

“Makubaliano haya mapya yanadhihirisha dhamira ya pamoja ya kampuni hizi mbili ya kulinda ubunifu wa binadamu na sanaa, ikiwemo kuhakikisha kwamba wasanii na waandishi wa nyimbo wanalipwa kwa haki, tunatangaza makubaliano haya mapya ya muda wa miaka kadhaa ambayo yataboresha zaidi fursa za ubunifu na kibiashara kwa wasanii wa UMG na waandishi wa nyimbo wa Universal Music Publishing Group (UMPG)” imesema taarifa hiyo

Hata hivyo Universal Music Group, imeweka wazi kuwa wapo ili kuunda utamaduni kupitia nguvu ya Sanaa huku Meta ikijenga teknolojia zinazosaidia watu kuungana kupitia jamii, na kukuza biashara ambapo kwa pamoja wamedai kuwa lengo lao kubwa ni kuleta vyanzo vipya vya mapato kwa wasanii na waandishi wa nyimbo.

Utakumbuka kuwa mara ya kwanza kampuni hizi mbili kuingia makubaliano ilikuwa mwaka 2017 ambapo walianzisha ushirikiano wao katika mtandao wa Facebook na badaye Instagram.

Wasanii ambao wapo chini ya Universal Music Group na ngoma zao zitasikilizwa WhatsApp ni pamoja na Billie Eilish, Taylor Swift, Adele, Drake na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags