Ngannou apigwa kwa  K.O, Joshua amtaka asiache ngumi

Ngannou apigwa kwa K.O, Joshua amtaka asiache ngumi

Bondia maarufu kutoka nchini Cameroon Francis Ngannou amechapwa na Anthony Joshua kwa kumpiga Knock Out (K.O) katika pambano la uzito wa juu lililofanyika Riyadh, Saudi Arabia usiku wa kuamkia leo.

Joshua ambaye ni Bingwa wa zamani wa uzito wa juu alimuangusha bingwa wa zamani wa UFC, Ngannou katika raundi ya kwanza na baadae kumuangusha tena raundi ya pili jambo ambalo lilisababisha mwamuzi kumaliza pambano hilo.

Huu unakuwa ushindi wa nne mfululizo kutoka kwa Joshua, lakini kwa upande wa Francis Ngannou litakuwa ni pambano lake la pili kupoteza mfululizo, kwani mwishoni mwa mwaka jana alipoteza pambano dhidi ya Tyson Furyhe ambapo #Tyson alishinda kwa point.

Aidha baada ya pambano hilo kutamatika Anthony Joshua alitoa ushauri kwa bondia mwenzake ambapo alimwambia kuwa asijiskie kukata tamaa kwani yeye ni bondia mzuri na anauwezo mkubwa kupigwa K.O sio mwisho wa dunia hivyo basi kinachotakiwa ni Ngannou kurudi kujifunza na kujiboresha ili arudi tena ulingoni akiwa imara.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags