Ndege ya kivita ya Urusi yasababisha uharibifu mji wa Belgorodi

Ndege ya kivita ya Urusi yasababisha uharibifu mji wa Belgorodi

Ndege ya kivita aina ya Su-34 ilirusha bomu la anga kwa bahati mbaya, baada ya kushambulia mji wa Belgorodi inasemekana haikuwa na lengo la kusababisha maafa hayo.

Tukio hilo lilitokea saa nne usiku siku ya Alhamisi kuamkia Ijumaa. Wizara ya ulinzi mjini Moscow ilithibitisha kuwa ndege ya kivita ya Urusi ilishambulia kwa bahati mbaya katika mji huo ulioko karibu na mpaka wa Ukrane.

Jiji la Belgorod lenye Zaidi ya watu 370,000 pia liko karibu maili 25 kilomita 40 kutoka mpaka wa Ukraine watu hao wamekuwa wakiishi kwa hofu ya mashambulizi ya makombora ya Ukraine tangu Urusi iivamie Ukraine mwaka jana na ndege za Urusi pia huonekana mara kwa mara kwenye anga la jiji hilo.

Aidha Gavana wa eneo la Vyacheslav Gladkov alisema shambulio hilo limesababisha shimo kubwa lenye upana wa takriban mita 20 katikati mwa jiji, na katika ajali hiyo wanawake wawili wamejeruhiwa na majengo kadhaa kuharibiwa vibaya, alisema Gavana huyo






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post