Nay Wa Mitego Aitwa Basata

Nay Wa Mitego Aitwa Basata

Msanii wa muziki Bongo Nay Wa Mitego ameitwa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kufuatia wimbo wake wa ‘Nitasema’.

Nay kupitia ukurasa wake wa Instagram ameweka wazi kuwa amepokea barua ya wito kutoka Basata kwa lengo la kwenda kujadili wimbo wake mpya.

“Nimepokea barua ya wito kutoka Baraza La Sanaa Taifa, Basata. kufika kwenye kikao kujadili wimbo wangu wa 'Nitasema' kikao kilipangwa kufanyika leo asubuhi but nilikua safarini, so kesho Ijumaa saa sita mchana nitafika ofisi za Basata kuitikia wito huo.

“Mashabiki wangu na Watanzania wapenda haki wote kwa ujumla mimi na nyinyi letu ni moja na tutashinda kwenye kila jaribu coz sauti ya wengi ni sauti ya Mungu na haki huinua taifa. Nitasema ata iweje bado,” ameandika Nay

Mpaka kufikia sasa wimbo huo wa ‘Nitasema’ wa Nay aliyomshirikisha Raydiace umefikisha zaidi ya watazamaji 598,045 kupitia mtandao wa Youtube.

Hata hivyo utakumbuka baada ya kutoa wimbo huo, msanii huyo alianza kuchangiwa fedha kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wadau wa muziki wakidai kuwa ni zawadi yake kwa kuwa ameimba mambo yanayogua jamii






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags