Nandy: Sipendi marafiki wa mume wangu.

Nandy: Sipendi marafiki wa mume wangu.

Ebwana eeeh!! Katika hali isiyo ya kawaida bwana, kama ambavyo mnafahamu kipindi ambacho mwanamke anakua mjamzito kila mmoja huwa kuna tabia ambazo anakua nazo.

Licha ya hayo inawezekana kabisa akawa na tabia ambazo hakua nazo hapo awali lakini baada ya kuwa mjamzito hua anakua tofauti kidogo.

Sasa bwana mke wa Billnass, Nandy yeye amefunguka tabia ambazo anazo kwa sasa kutokana na hali ambayo yuko nayo.

Kupitia mahojiano aliyofanyiwa na chombo cha habari amesema kuwa kwa sasa anatabia ya kuchukia marafiki wa mume wake Billnass.

“Hahaha Its wierd, sipendi marafiki wa mume wangu yaani jamani naomba mnisamehe tu imetokea tu kutoelewana nao wakipiga simu napokea mimi, nawaambia ache analea mimba, yaani kuna wakati huwa nazingua kabisaa,” Nandy.

“Kipindi cha mwanzo nilikua nalia bila sababu hata kwa jambo dogo tu naona nimeonewa naweza kulia hata siku mbili sitaki chochote hadi alipoambiwa kuwa ni mimba ndo akawa anaelewa sasa.”

Haya msomaji wa Mwanachi scoop dondosha comment yako kwenye hili bhana unaonaje?

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags