Mwili wa Mtanzania aliyefariki Ukraine wawasili nchini

Mwili wa Mtanzania aliyefariki Ukraine wawasili nchini

Ndugu na jamaa wa Mtanzania Nemes Tarimo aliyefariki nchini Ukraine wamepokea mwili wa kijana huyo leo alfajiri katika uwanja wa ndege, Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa familia, kijana huyo ataagwa kisha kusafirishwa kwa ajili ya maziko Nyanda za juu kusini mwa Tanzania.

Mapema wiki hii serikali ya Tanzania ilithibisha kijana huyo kuuawa vitani Ukraine mara baada ya kufungwa kwa uhalifu nchini Urusi na baadae kujiunga na kundi la mamluki wa Urusi , Wagner.

Nemes Tarimo alienda nchini Urusi kwa ajili ya masomo ya juu kabla ya kupatwa na umauti wake.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags