Mwandishi Victoria Amelina afariki dunia

Mwandishi Victoria Amelina afariki dunia

Mwandishi maarufu wa Ukraine, Victoria Amelina amefariki dunia leo Jumatatu kutokana na majeraha aliyopata kufuatia shambulio la kombora lililotokea Jumanne alipokuwa akipata chakula katika eneo la Ria Lounge ambapo takriban watu wengine 60 walijeruhiwa.

Victoria mwenye umri wa miaka 37 ambaye ni mtafiti wa uhalifu wa kivita anakuwa mtu wa 13 kufariki katika shambulio hilo la kombora lililogonga mgahawa katika mji wa mashariki wa Kramatorsk ulioko chini ya udhibiti wa Ukraine, eneo ambalo linalo karibiana na sehemu zinazokaliwa na Russia.

Aidha Chama cha waandishi nchini Ukraine kimesema madaktari walifanya kila wawezalo kuokoa maisha ya Victoria lakini kwa bahati mbaya jeraha hilo lilikuwa baya, huku wanaharakati wa haki za binadamu wakitaja shambulio hilo kuwa uhalifu wa kivita.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags