Mwanaume ukitaka kuishi maisha marefu epuka Mwanamke wa aina hii

Mwanaume ukitaka kuishi maisha marefu epuka Mwanamke wa aina hii

Oooooohoooooh! I hope mko good sana watu wangu wa nguvu haya sasa leo kwenye mahusiano yani kama kawaida yetu tunakuletema mada ambazo zitakujuza mambo kadha wa kadha.

Wewe kijana ambae unataka kuingia kwenye mahusiano ama kwenye ndoa ungana nasi kujua njia mbalimbali ambazo zitakusaidia katika mahusiano yako na kukujuza kuwa nani ni sahihi kwako na nani si sahihi.

Kuna aina ya wanawake wa kuwaepuka kama unataka kuishi muda mrefu katika maisha yako, kwasababu wapo baadhi ya wanawake ukiwaweka karibu na maisha yako hakuna hata siku moja ambayo utakuja kuishi kwa amani kutokana na matukio ambayo atakufanyia.

  1. Mwanamke Mwenye Mahusiano Na Wanaume Wengine

Hata siku moja usije ukajaribu kuwa na mwanamke wa aina hii ambaye ana mahusiano na wanaume wengine, yaani haridhiki na wewe peke yako, anaweza kukufanya uishi kwenye ndoa isiyo na furaha.

Tafuta mwanamke ambaye analidhika na wewe kutokana na maisha yako hana tamaa wala hachepuki na wanaume wengine, ila ukijichanganya ukawa na mwanamke ambaye hajatulia utakufa mapema kwa mawazo.

  1. Mwanamke anayehitaji pesa kutoka kwako ili atumie vitu vyake bila kukuonyesha mapenzi ya kweli.

Wanawake wengine wanategemea wanaume zao kwenye kila kitu, yaani hajali unazo au hauna kiujumla hana huruma na kisingizio ni kwamba kwakuwa unampenda basi utahitajika kutimiza kila hitaji lake, mwanamke wa aina hii anaweza kukurudisha nyuma kimaendeleo.

Tafuta mwanamke ambaye atakusaidia kutimiza malengo yako na siyo kukurudisha nyuma ukiona yeye siku zote anakurudisha tu nyuma fanya kila linalowezekana kuepukana nae

  1. Mwanamke asie kuheshimu na anaekukimbia ukiumwa

Siku zote mapenzi ni kuvumiliana kwenye nyakati zote yaani shida na raha, wapo wanawake ambao akiskia unaumwa basi kama sio nayeye ataumwa basi atapata safari ya ghafla na kukuacha ukiwa unaumwa, mwanaume oa mwanamke ambaye atakujari ukiwa unaumwa pamoja na matatizo.

Kwenye swala la kukuheshimu angalia mwanamke ambae anakuskiliza katika kila jambo, heshima ndo kila kitu katika mahusiano hakuna mahusiano yanaweza kudumu bila heshima au kuheshimiana.

4.mwanamke anaekufananisha na wanaume wengine

Hakuchukuli ulivyo usioe mwanamke wa aina hii ambaye hatosheki na ulichonacho na ambaye haridhiki na wewe, muda wotw anaishinda akisifia wanaume wengine ambaye ni bora kukuzidi

  1. mwanamke asiye na muda na wewe

Mwanamke mzuri ni yule anaetumia muda wake na wewe kwenye kuongea kuhusu maendeleo yenu, kama hana muda nawewe usipoteze muda wa kuwa nae. Hawezi kukusaidia katika maisha yako

  1. mwanamke mvivu

Ili ufanikiwe katika maisha ni lazima uwe na mwanamke mchapakazi ili akupe sapoti na kukupa moyo katika kazi zako lakini endapo utaoa mwanamke ambaye yeye akiamka moja kwa moja kwenye TV hafikirii kesho yenu itakuwaje yeye anaiwaza leo tu huyo sio mwanamke wa kuoa atakupa mawazo utakufa mapema.






Comments 1


  • Awesome Image
    Balikeka Andrea

    Pia usioe mwanamke ambaye Shida yake anaifanya iwe shida yenu wote ila shida yako Wewe anaifanya kuwa yako peke yako. Mwanamke wa hivo mwiba mkali epukana naye

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags