Mtoto wa siku 4 akutwa kwenye shimo la choo

Mtoto wa siku 4 akutwa kwenye shimo la choo

Mtoto mchanga aliyetupwa kwenye choo cha shimo na mtu asiyejulikana huko Kisii nchini Kenya alikuwa akilia sana nakupelekea umma kujua huyo mtoto analia kuotokea wapi.

Kulingana na huduma ya Kitaifa ya Polisi maafisa kutoka kiituo cha polisi cha Roma walichukua hatua kufuatilia ripoti iliyotolewa na mwananchi kwamba kulikuwa na kilio cha mtoto mchanga kutoka kwenye choo.

Polisi nchini humo walifika kwa haraka katika kanisa katoliki la Roma baada ya kuitwa na kufanikiwa kumwokoa malaika huyo kisha baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Marani Level 4 na kukabidhwa kwa afisa Mkuu Muuguzi  na mtoto huyo akiwa na afya njema kabisa.

“Afisa Mkuu wa kituo na maafisa wengine kutoka kituo cha Roma walifika haraka katika eneo la tukio kwa takriban kilomita 1.4 kutoka kituoni hapo walibomoa choo cha shimo na kumuokoa mtoto wa kike anayekadiriwa kuwa na siku nne” ilisema alisema NPS mtu wa ulinzi wa watoto

Aidha NPS alieleza kuwa atamshughulikia mtoto huyo kupitia kitengo chake maalum cha ulinzi wa Watoto na kumpongeza mwananchi alie toa taarifa zilizo fanikisha kuokolewa mtoto huyo akiwa salama.

Chanzo TUKO






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags