Mtoto wa Diddy aanza kurithi vitu vya baba yake

Mtoto wa Diddy aanza kurithi vitu vya baba yake

Mtoto wa mkali wa Hip hop kutoka Marekani, Diddy, Christian Combs, maarufu kama King Combs taratibu ameanza kurithi vitu vya baba yake jambo ambalo liliwashitua mashabiki huku baadhi yao wakidai kuwa sio sawa.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Diddy, King Combs ameshare video akieleza kuwa kwasasa ndio ataishikiria akaunti ya baba yake ya Instagra mpaka hapo atakupo kuwa huru. “Yo, vipi watu? Ni King Combs. Na kwa sasa, nashikilia akaunti ya Instagram ya pops wangu.”

Aidha kijana huyo ameleza kuwa nia ya kushikilia akaunti ya baba yake ni kuanza kusambaza matukio chanya, yenye mafanikio na mazuri ambayo baba yake amewahi kuyafanya katika jamii na kwenye tasnia ya muziki wa Hip hop nchini Marekani.

Hata hivyo kufuatiwa na video hiyo baadhi ya mashabiki wameibuka katika upande wa komenti wakimchokoza mtoto huyo kwa kudai kuwa ameanza kurithi vitu vya baba yake mapema kabla ya kuhukumiwa huku wengi wao wakimpongeza kwa hatua hiyo.

Utakumbuka Diddy alikamatwa na kutupwa gerezani Septemba 16 jijini Ney York kwa makosa makubwa ya unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wawatu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Me 5, 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags