Mtoto atolewa vyuma 52 tumboni

Mtoto atolewa vyuma 52 tumboni

Mama wa mtoto mvulana mwenye umri wa miaka mitano ambaye alinusurika kifo baada ya kumeza vyuma 52 kutoka kwenye kifaa cha kuchezea amewaonya wazazi dhidi ya kununua baadhi ya michezo ya watoto kwani inaweza kusababisha hatari.

Daktari alilazimika kupasua tumbo la mtoto Jude sehemu tano ili kuondoa vyuma vilivyokua vimekwama tumboni mwake .

Mama wa mtoto Bi Foley, mwenye umri wa miaka 34, alisema alianza kuwa na wasiwasi baada ya mtoto wake kushindwa kupona baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Baada ya kuongezeka kwa wasiwasi, mwezi Agosti alimpeleka Jude katika hospitali akiwa na maumivu makali ya tumbo.

Uchunguzi na kipimo cha X-ray kilibaini kuwa alikuwa na vyuma tumboni.

Wizara ya afya ya Wales (PHW) imetoa wito kwa watu kuwa makini na kufikiria kabla ya kununua bidhaa kwa ajili ya watoto wao zenye vyuma vidogo na betri na vifungo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags