Mtengeneza filamu Toru Kubota ahukumiwa jela miaka 10 Myanmar

Mtengeneza filamu Toru Kubota ahukumiwa jela miaka 10 Myanmar

Utawala wa kijeshi nchini Myanmar umemfunga jela miaka 10 mtengeneza filamu Toru Kubota ambae ni raia wa Japan. Hii ni baada ya kukamatwa zaidi ya miezi miwili iliyopita wakati akipiga picha za maandamano ya kupinga mapinduzi.

Kubota mwenye umri wa miaka 26 alizuiliwa karibu na maandamano ya kuipinga serikali katika kitovu cha kibiashara cha Yangon mwezi Julai pamoja na raia wawili wa Myanmar.

Msemaji wa serikali ya kijeshi amesema alihukumiwa jana kifungo cha miaka saba jela kwa kuvunja sheria inayoharamisha usambazaji wa taarifa zinazoweza kuhujumu usalama wa taifa, amani na utulivu.

Pia alipewa kifungo cha miaka mitatu kwa kuhimiza upinzani dhidi ya jeshi, mashitaka ambayo yametumiwa sana na watawala wa kijeshi katika ukandamizaji unaofanywa nchini humo dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari tangu mapinduzi ya mwaka jana.

Vifungo hivyo vitatekelezwa kwa wakati mmoja.

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags