Mke wa Hakimi aambulia patupu baada ya talaka

Mke wa Hakimi aambulia patupu baada ya talaka

Ebanaa wee!! vitabu vya dini vinasema wanaweke ishini nao kwa akili msemo huu una thibiti kwa mke wa Ashraf Hakimi mchezaji wa klabu ya PSG,  aliefahamika kwajina la Hiba Abouk ameiambia mahakama kua anahitaji talaka huku akiiomba mahakama kumpa fungu la mali wagawane sawa sawa na mume wake.

Hakimi alikubali kutoa talaka lakini mahakama ilipochunguza vizuri chakushangaz na kumuacha mdomo wazi mwanamke huyo kuwa kwenye mali za mchezaji huyo walikuta hamiliki kitu hata kimoja hata benki yake hamna hata thumni.

Iligundulika kua Hakimi alijua kama hayo yatatokea ndio akaamua mali zake zote yaani pesa majumba na magari viandikwe kwa jina la mama yake mzazi ili isemekane kua mama yake ndio mmiliki halali wa mali zake.

Aidha mbali na Hakim mchezaji mwingine ambaye aliwahi kufanya hivi ni staa wa zamani wa Ghana Asamoah Gyan ambaye aliweka mali zake chini ya jina la kaka yake hivyo baada ya kuachana na mkewe alibakiwa na mali kidogo ingawa pesa zote zilikombwa na kubakiwa na Pauni 600 tu kwenye akaunti yake ya benki.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags