Miami Beach yafuta Sean Diddy Combs Day

Miami Beach yafuta Sean Diddy Combs Day

Uongozi wa Miami Beach umeondoa siku maalumu ya ‘rapa’ Diddy ambayo ilizinduliwa kwa mara ya kwanza Oktoba 13, 2016, huku sababu ikitajwa ni kufuatia na video ya Combs ikimuonesha akiwa nampiga aliyekuwa mpenzi wake cassie.

Kwa mujibu wa gazeti la Miami Herald limeripoti kuwa uongozi wa beach hiyo ulifanywa siku ya Jumatano wiki umeeleza kuwa ulichukua uamuzi huo kulinda usalama na ustawi wa jamii yao.

“Baada ya kutafakari, Meya na Tume ya Jiji wameamua kwamba imeondoa 'Siku ya Sean Diddy Combs' iliyozinduliwa kwa mara ya kwanza Oktoba 13, 2016, ili kulinda maadili ya Jiji letu, ustawi wa jamii, na heshima”

Mapema mwezi Mei rininga ya Cnn ilivujisha video Mkali wa Hip-hop Diddy ikimuonesha akimpiga mpenzi wake wa zamani Cassie ambapo tukio hilo linadaiwa kutokea mwaka 2016.

Aidha kufuatiwa na video hiyo ya Mei 19, 2024 Diddy aliomba radhi kwa kile kilichotokea huku akidai kuwa hakuwa kwenye utimamu wa akili na yuko tayari kwenda kupatiwa msaada wa kisaikolojia ili kuwa mtu mwema.

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi za biashara ya ngono na unyanyasaji wa kijinsia tangu Novemba mwaka jana huku aliyekuwa mtayarishaji wa kazi zake Rodney "Lil Rod" Jones akidai kuwa #Combs alikuwa akiandaa sherehe za biashara ya ngono.

Aidha licha ya kufunguliwa kesi saba mpaka sasa lakini bado hakuna ushahidi madhubuti wa kumtia nguvuni mwanamuziki huyo huku baadhi ya mastaa akiwemo Suge Knight wakidai kuwa #Diddy ni #FBI.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags