Miaka 21 jela kwa kuiba Mbwa

Miaka 21 jela kwa kuiba Mbwa

Hii bwana imetokea huko nchini Marekani ambapo Mahakama ya Los Angeles, imemuhukumu James Howard Jackson ( 20) kifungo cha miaka 21 jela kwa kosa la kumjeruhi kwa risasi Ryan Fischer, ambaye ni muangalizi wa mbwa wa staa wa muziki wa Pop duniani Lady Gaga.

Jackson alishtakiwa kwa kosa la kujeruhi kwa risasi na kuiba mbwa wawili wa Lady Gaga, Koji na Gustav mwaka jana akiwa na wenzake wawili lakini mahakama ikamuacha huru kwa kile walichodai ni makosa yalitokea kwa maafisa wa mahakama.

Jackson alitekeleza shambulio hilo wakati muangalizi wa mbwa wa Lady Gaga akiwa anawatembeza mbwa wa staa huyo katika mitaa ya Los Angeles nchini Marekani.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Lady Gaga alitangaza ofa ya zawadi ya dola za Kimarekani 500,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni moja za Kibongo kwa yeyeto atakayefanikisha kupatikana kwa mbwa wake walioibwa, lakini mwanamke aliyewafikisha mbwa hao alishtakiwa kwa kosa la kuhusika na wahalifu na kupokea mali za wizi.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags